FAIDA ZA PROGRAM YA
“MPENZI WA KWELI DAIMA NI
ELIMU”
Program ya MPENZI WA KWELI DAIMA NI
ELIMU ni program ya kwanza ya aina yake ambayo itakuwa na faida kubwa nyingi
kwa Taifa wanufaika wa kwanza wakiwa wanafunzi na familia zao na hatimaye jamii
nzima. Program hii inatekelezwa mashuleni kwa ridhaa ya wazazi na uongozi wa
shule ambao wako tayari kupambana na tatizo ama janga kubwa la mmomonyoko wa
maadili kwa vijana waliopo masomoni. Program hii inahusisha Mafunzo kwa
wanafunzi, kitabu cha Mpenzi Wa Kweli Daima Ni Elimu, Poster ya Mpenzi Wa Kweli
Daima Ni Elimu na bango kubwa la Mpenzi Wa Kweli Daima Ni Elimu.
Ifuatayo ni orodha ya faida ya
program hii;
1. Kujitambua: Programu hii itasaidia Vijana hususani wanafunzi kujitambua, kutambua changamoto na hatari zilizopo mbele yao na jinsi ya kukabiliana
nazo.
2. Kuongeza UfauIu: Program
itasaidia kuinua Ari ya Kusoma,
kupunguza utoro wa wanafunzi
na atabia za kijinga, kuongeza
ufaulu mashuleni na kusaidia
kuinua kiwango cha elimu kitaifa.
3. Mimba na utoaji Mimba: Programu
hii itasaidia kukabiliana na tatizo la mimba mashuleni, utoaji mimba na vifo vya sirisiri vitokanavyo na utoaji mimba
unaofanywa kwa siri na wasichana wengi bila wazazi ama walezi wao kufahamu.
4. Kukabiliana na Ukimwi: Programu
hii itasaidia kukabiliana na tatizo la ongezeko la Maradhi hatari ya UKIMWI kwa
wanafunzi na kwa jamii kwa ujumla.
5. Vifo vya Uzazi: Programu
hii itasaidia kupunguza vifo
vya akina
mama vinavyosababishwa na uzazi katika umri mdogo.
6. Watoto wa Mitaani: Programu hii itasaidia kupunguza tatizo la watoto wa mitaani linalotokana
na wazazi wa kike hasa wenye umri mdogo kutelekezwa na kushindwa kulea watoto na kupunguza
idadi ya wazazi wanaozaa kabla ya kujiandaa vizuri kimaisha.
7. Uhalifu na Uchangudoa: Programu
hii itasaidia kupunguza vijana wanaojiingiza katika uhalifu
wa aina
mbali mbali kama vile wizi na
ujambazi kwani idadi ya vijana watakaokuwa wanashindwa masomo na kujiingiza
katika vitendo viovu itapungua. Pia iitasaidia kupunguza idadi ya wasichana
kujiingiza katika maisha ya uchangudoa kwani idadi ya wasichana watakaoshindwa
masomo na kujiingiza katika vitendo viovo itapungua
8. Kupunguza Gharama za Kusomesha: Programu
hii itasaidia kupunguza gharama zinazowakabili wazazi kwasababu wanafunzi wengi wataacha matumizi
mabovu ya
fedha wanazopewa
na wazazi kwa ajili ya masuala ya elimu.
9. Utapeli wanaofanyiwa wazazi: Programu hii itasaidia kupunguza
wimbi la
wanafunzi kupeleka
nyumbani
sababu za uongo ili kujipatia fedha
za ziada kwa ajili ya mambo ya anasa.
10.Kupunguza umasikini katika jamii: Programu hii itasaidia kupunguza umasikini
katika familia nyingi kwakuwa watoto wao watakuwa na bidii katika masomo na
hatimaye kufanikiwa katika elimu na hata watakao kwama watakuwa katika afya
nzuri itakayowasaidia kushiriki vizuri maendeleo na uchumiwa familia zao.
11.Kuimarisha Benki ya Damu:
Watu wengi huogopa kujitolea Damu kwa dhana wanaweza kupimwa UKIMWI na kujikuta
wana maambukizi (Hawajiamini). Programu hii itasaidia kuongeza idadi ya watu
ambao watakuwa tayari kujitolea damu, kwani idadi ya vijana ambao wataishi bila
hofu itaongezeka kwakuwa kitabu kitakuwa kimewaondoa vijana wengi katika maisha
yanayochangia maambukizi ya UKIMWI.
12.Kuokoa fedha za Serikali: Serikali
inatumia fedha nyingi sana katika kugharimia matibabu ya maradhi
yanayosababishwa na UKIMWI. Programu hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza
maradhi hayo na hatimaye kupunguza mzigo wa Serikali katika kupambana na
maradhi hayo.
13.Pato la Taifa na Ukuaji wa Uchumi wa Nchi: Programu hii itasaidia ukuaji wa
pato la Taifa, uchumi na maendeleo kwa ujumla kwakuwa mambo mengi
yatakayoepukwa nilitoeleza hapo nyuma ni mambo yanayochangia katika kuipa
Serikali mzigo mkubwa wa matumizi. Programu hii itasaidia idadi ya vijana na
watanzania kwanza kuwa wenye elimu nzuri na pili wenye afya na nguvu za
kuchangia amaendeleo na uchumi wa Taifa lao.
14.Kupungua Migogoro katika jamii: Programu hii itasaidia kupunguza migogoro mingi katika jamii kwani mingi kati ya
migogoro inayotokea katika jamii inasababishwa na ndoa za utotoni, mahusiaono
ya kimapenzi ya watoto nk. Kupungua kwa hayo kutasaidia kupungua kwa migogorto
katika jamii. Aidha migogoro pia huiongezea Serikali mzigo wa matumnizi.
FALSAFA YA PROGRAM YA MPENZI WA KWELI DAIMA NI ELIMU
Programu hii ina falsafa Zifuatazo;
1. Kufundisha: Falsafa ya Programu hii inafundisha.
2. Kushauri: Falsafa ya kitabu hiki
inashauri.
3. Kuadhibu: Falsafa ya Programu hii inatoa adhabu hasa kwa
vijana ambao wanakusudia kuendelea na tabia zao bila kujali kuwa wameonywa, na pia kwa vijana ambao wanataka kuingia
kwenye tabia hizo bila kujali kuwa wameonywa.
4. Kutia hofu: Falsafa ya Programu hii inatia hofu vijana, hofu ambayo inakusudia kuwakwepesha vijana
hatari ziliyopo mbele yao.
5. Kuaibisha: Falsafa ya
Programu hii inakusudia kuwafanya
wanafunzi walio
katika mahusiano ya kimapenzi waoneane aibu kutokana na
vitendo vyao
na wale ambao hawajawa na tabia hizo waone aibu kujiingiza katika tabia hizo.
Kwa maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kushiriki program hii na namna
ya uchangiaji
Tuma Email
utatumiwa maelekezo
By
Jacob Malihoja
MKURUGENZI
TUBADILIKE INVESTMENTS