Sunday, December 6, 2015

MPENZI WA KWELI DAIMA NI ELIMU



FAIDA ZA PROGRAM YA
“MPENZI WA KWELI DAIMA NI ELIMU”

 
Program ya MPENZI WA KWELI DAIMA NI ELIMU ni program ya kwanza ya aina yake ambayo itakuwa na faida kubwa nyingi kwa Taifa wanufaika wa kwanza wakiwa wanafunzi na familia zao na hatimaye jamii nzima. Program hii inatekelezwa mashuleni kwa ridhaa ya wazazi na uongozi wa shule ambao wako tayari kupambana na tatizo ama janga kubwa la mmomonyoko wa maadili kwa vijana waliopo masomoni. Program hii inahusisha Mafunzo kwa wanafunzi, kitabu cha Mpenzi Wa Kweli Daima Ni Elimu, Poster ya Mpenzi Wa Kweli Daima Ni Elimu na bango kubwa la Mpenzi Wa Kweli Daima Ni Elimu.

Ifuatayo ni orodha ya faida ya program hii;
1.     Kujitambua: Programu hii itasaidia Vijana hususani wanafunzi kujitambua, kutambua changamoto na hatari  zilizopo mbele yao na jinsi ya kukabiliana nazo.
2.     Kuongeza UfauIu: Program itasaidia kuinua Ari ya Kusoma, kupunguza utoro wa wanafunzi na atabia za kijinga, kuongeza ufaulu mashuleni na kusaidia kuinua kiwango cha elimu kitaifa.
3.     Mimba na utoaji Mimba: Programu hii itasaidia kukabiliana na tatizo la mimba mashuleni,  utoaji mimba na vifo vya sirisiri vitokanavyo na utoaji mimba unaofanywa kwa siri na wasichana wengi bila wazazi ama walezi wao kufahamu.
4.     Kukabiliana na Ukimwi: Programu hii itasaidia kukabiliana na tatizo la ongezeko la Maradhi hatari ya UKIMWI kwa wanafunzi na kwa jamii kwa ujumla. 
5.     Vifo vya Uzazi: Programu hii itasaidia kupunguza vifo vya akina mama vinavyosababishwa na uzazi katika umri  mdogo.
6.     Watoto wa Mitaani: Programu hii itasaidia kupunguza tatizo la watoto wa mitaani linalotokana na wazazi wa kike hasa wenye umri mdogo kutelekezwa na kushindwa kulea watoto na kupunguza idadi ya wazazi wanaozaa kabla ya kujiandaa vizuri kimaisha.
7.     Uhalifu na Uchangudoa: Programu hii itasaidia kupunguza vijana wanaojiingiza katika uhalifu wa aina mbali mbali kama vile wizi na ujambazi kwani idadi ya vijana watakaokuwa wanashindwa masomo na kujiingiza katika vitendo viovu itapungua. Pia iitasaidia kupunguza idadi ya wasichana kujiingiza katika maisha ya uchangudoa kwani idadi ya wasichana watakaoshindwa masomo na kujiingiza katika vitendo viovo itapungua
8.    Kupunguza Gharama za Kusomesha: Programu hii itasaidia kupunguza gharama zinazowakabili wazazi kwasababu wanafunzi wengi wataacha matumizi mabovu ya fedha wanazopewa na wazazi kwa ajili ya masuala ya elimu.
9.    Utapeli wanaofanyiwa wazazi: Programu hii itasaidia kupunguza wimbi la wanafunzi kupeleka nyumbani sababu za uongo ili kujipatia fedha za ziada kwa ajili ya mambo ya anasa.
10.Kupunguza umasikini katika jamii: Programu hii itasaidia kupunguza umasikini katika familia nyingi kwakuwa watoto wao watakuwa na bidii katika masomo na hatimaye kufanikiwa katika elimu na hata watakao kwama watakuwa katika afya nzuri itakayowasaidia kushiriki vizuri maendeleo na uchumiwa familia zao.
11.Kuimarisha Benki ya Damu: Watu wengi huogopa kujitolea Damu kwa dhana wanaweza kupimwa UKIMWI na kujikuta wana maambukizi (Hawajiamini). Programu hii itasaidia kuongeza idadi ya watu ambao watakuwa tayari kujitolea damu, kwani idadi ya vijana ambao wataishi bila hofu itaongezeka kwakuwa kitabu kitakuwa kimewaondoa vijana wengi katika maisha yanayochangia maambukizi ya UKIMWI.
12.Kuokoa fedha za Serikali: Serikali inatumia fedha nyingi sana katika kugharimia matibabu ya maradhi yanayosababishwa na UKIMWI. Programu hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maradhi hayo na hatimaye kupunguza mzigo wa Serikali katika kupambana na maradhi hayo.  
13.Pato la Taifa na Ukuaji wa Uchumi wa Nchi: Programu hii itasaidia ukuaji wa pato la Taifa, uchumi na maendeleo kwa ujumla kwakuwa mambo mengi yatakayoepukwa nilitoeleza hapo nyuma ni mambo yanayochangia katika kuipa Serikali mzigo mkubwa wa matumizi. Programu hii itasaidia idadi ya vijana na watanzania kwanza kuwa wenye elimu nzuri na pili wenye afya na nguvu za kuchangia amaendeleo na uchumi wa Taifa lao.
14.Kupungua Migogoro katika jamii: Programu hii itasaidia kupunguza migogoro mingi katika jamii kwani mingi kati ya migogoro inayotokea katika jamii inasababishwa na ndoa za utotoni, mahusiaono ya kimapenzi ya watoto nk. Kupungua kwa hayo kutasaidia kupungua kwa migogorto katika jamii. Aidha migogoro pia huiongezea Serikali mzigo wa matumnizi.

FALSAFA YA PROGRAM YA MPENZI WA KWELI DAIMA NI ELIMU
Programu hii ina falsafa Zifuatazo;
1.     Kufundisha: Falsafa ya Programu hii inafundisha.
2.     Kushauri: Falsafa ya kitabu hiki inashauri.
3.    Kuadhibu: Falsafa ya Programu hii inatoa adhabu hasa kwa vijana ambao wanakusudia kuendelea na tabia zao bila kujali kuwa wameonywa, na pia kwa vijana ambao wanataka kuingia kwenye tabia hizo bila kujali kuwa wameonywa.
4.     Kutia hofu: Falsafa ya Programu hii inatia hofu vijana, hofu ambayo inakusudia kuwakwepesha vijana hatari ziliyopo mbele yao.
5.    Kuaibisha: Falsafa ya Programu hii inakusudia kuwafanya wanafunzi walio katika mahusiano ya kimapenzi waoneane aibu kutokana na vitendo vyao na wale ambao hawajawa na tabia hizo waone aibu kujiingiza katika tabia hizo.

 Kwa maelezo zaidi juu ya utaratibu wa kushiriki program hii na namna ya uchangiaji

Tuma Email
 utatumiwa maelekezo

By  
Jacob Malihoja
MKURUGENZI
TUBADILIKE INVESTMENTS

No comments:

Post a Comment