Thursday, May 7, 2009

Mnara wa Kumbukumbu ujengwe kwa ajili ya Mabomu ya Mbagala

Kutokana na uzito wa matukio ya milipuko ya mabomu Mbagala, ingependeza askari walikufa wakiwa kazini watambuliwe kuwa ni Mashujaa. Aidha wananchi wote waliokufa kutokana na milipuko hiyo nao wanastahili kutambuliwa kuwa ni mashujaa kwani walikufa kutokana na milipuko ya silaha za kivita kutokana na ajali ya kijeshi, jeshi linalowalinda wakati wananchi hao nao wakiwa katika harakati zao za kawaida za kulijenga Taifa.

Kutokana na ukweli huo katika mazingira mengine Serikali ina kila sababu ya kujenga mnara wa kumbu kumbu ya tukio hilo la kutisha kando ya barabara ya Kilwa kwenye eneo la Jeshi, mnara ambao mashujaa wanajeshi kwa raia waliokufa katika tukio hilo wataorodheshwa majina yao.

Hii inatokana na ukweli kwamba tukio hilo halikuwa la mzaha ni tukio lililopoteza maisha ya wananchi wengi na askari wetu. Ni tukio lililoleta hofu kwa wananchi zaidi ya milioni 4 wa jiji la dar es Salaam.

Kama ambavyo minara kadhaa ya kumbu kumbu imejengwa, tukio hili nalo linahitaji mnara. Hii itasaidia kuweka kumbu kumbu kwa vizazi vijavyo na kuwakumbuka marehemu ndugu zetu kila wakati.

2 comments: