Msichana mmoja Rehema Njelekela (19) mkazi wa kijiji cha Magagula wilaya ya Songea mkoani Ruvuma , anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kosa kumyonga mtoto wake na kisha kumfukia nje ya nyumba ya mama yake kwa kuhofia maisha magumu baada ya kutelekezwa na mpenzi wake anayeishi nchi jirani ya Msumbiji.
Rehema Njelekela akiwa Wodini katika Hospitali ya mkoa wa Ruvuma chini ya ulinzi wa polisi.
Namfahamu Binti huyu ambaye kwa sasa dunia ni nyekundu kwake, itategemea majaliwa ya mwenyezi mungu kurudi katika maisha yake ya kawaida. Hivi ni sahihi kuua mwanao kwasabu ya maisha magumu? nani wa kulaumiwa? Kwa Mtazamo wangu ni Mwanaume .. lakini hapana .. ni wote mwanaume asilimia 60 na msichana mwenyewe asilimia 40.
Matukio haya yananihamasisha kuharakisha kuandika kitabu changu kuhusu ukatili kwa wanawake na watoto.
Sijui niseme nini? Nashangaa ameitunza mimba miazi tisa na kujifungua na mwisho anafanya hivi kweli alikaza kwelikweli roho.
ReplyDeleteKimsingi Binti huyo alikosa ushauri nasaha, inawezekana alikumbana na wakati mgumu wa kimahusiano katika kipindi cha mwishoni mwa ujauzito .. na kujikuta hana majibu mengine ya matatizo yake zaidi ya kutoa uhai wa mtoto .. kwasababu ambazo kutokana na uwezo wake wa kufikiri ulipoishia inawezekana kwanza alitaka kuondokana kabisa na huyo mwanaume aliyempa mimba .. na ama kuondokana na kazi ya utunzaji ya mtoto wakati tayari ameshatofautiana na huyo aliyempa mimba. ndio maana nasema Mwanaume kwa namna moja au zaidi amehusika kwa kiwango kikubwa .. na kama mimi ningekuwa nashughulikia tatizo hilo .. ama matatizo kama haya mwanaume naye anatakiwa atiwe Mbaroni kwasababu ana mchango mkubwa kwa binti kufanya tukio hilo.
ReplyDelete