Wabunge Kuneni Vichwa kabla ya Kushabikia mambo
Kimsingi wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaoshabikia sakata la nauli ya kivuko wamechemsha, wamefikiria haraka na kutoa kauli kabla ya kutafakari kwa kina. Nashawishika kuamini kuwa wamesukumwa na mtazamo wa kisiasa na sio “facts” kwa lugha njyingine wanajipendekeza tu kwa wananchi bila kujali madhara ya hulka hiyo. Kwa mtazamo wangu waliomzomea Dr. Magufuli ni wahuni si wananchi wenye hekima zao, na kama si wahuni ni watu waliohamasishwa “motivated” na siasa. Sasa si jambo la kufurahisha kuona msomi na kiongozi anayetunga sheria na kujadili maendeleo ya nchi anaungana na watu washabiki ama wahuni wasio na nidhamu.
Kama walivyonukuliwa na mtandao wa NIFAHAMISHE “Hatukubaliani na ongezeko hilo kabisa kabisa, na Waziri aombe radhi wananchi pamoja na sisi wazawa kwani bei ya shilingi 100 imetumika kwa zaidi ya miaka 14 sasa, iweje leo ndio ionekane mapato hayapatikani,” kwa kauli kama hii Wabunge na wananchi waliozomea walipaswa kutafakari mishahara imeongezwa mara ngapi, Mafuta yamepanda mara ngapi, gharama za vipuri. Gharama zingine za uendeshaji nk zimepanda mara ngapi, hivi gharama hizo nazo zilisimama miaka yote tisa kama ilivyosimama nauli.
Wananchi wenye busara wangewakilisha maombi yao kwa ustaarabu huku wakiwa wamezingatia vigezo vya msingi.
Binafsi sikubaliani na hatua ya Mhe. Faustine Nduguline kumshitaki Waziri Dr. Magufuli kwa Maziri Mkuu, Mbunge alipaswa kuwaelimisha wananchi kwa lugha nzuri na yenye busara ikiwa walishindwa kumuelewa Waziri wake. Kwa uapenda mwingine nina imani kubwa kwa hekima alizonazo Waziri Mkuu Mizengo Pinda suala hilo litafanyiwa kazi kwa busara na hekima zaidi.
Labda naloweza kusema na kumlaumu Dr. Magufuli ni ku-over react jambo ambalo linatokana na udhaifu wa kibinadamu hasa unapotukanwa na watu unaowahangaikia.
Nikinuu mtandao wa NIFAHAMISHE “Wabunge hao walisema jiji la Dar es Salaam linachukua watu wengi kutoka Kigamboni hivyo, kupandisha nauli ni kuwaonea wananchi wanaoishi huko na Serikali inaonyesha kuwakandamiza wananchi waishio huko “
Mbagala ina watu wengi kuliko sehemu yoyote ya jiji la Dar es Salaam, Gongo la Mboto ina watu wengi kuliko Kigamboni na maeneo mengine yanachukua watu wengi Mbona nauli za daladala zimepanda mara kadhaa hawajamzomea kiongozi yeyote, hivi huko vijijini wanakolipa nauli sh. 200 kwa miaka kadhaa sasa wana fedha zaidi kuliko huku mjini na kwanini huku mjini wabebwe miaka yote? Hivi kuonewa na kukandamizwa ni Kigamboni pakeyake?
Hongera Azim Dewji, Vicent Michael na wote wanaomuunga Mkono Magufuli
Nimesoma katika gazeti la mwananchi na kukuta habari hii “Magufuli apata watetezi” mwanza nilifikiri nipo peke yangu nayemuunga mkono Dr. Magufuli.
“Dk Magufuli ameanza kupata watetezi baada ya mfanyabiashara maarufu nchini, Azim Dewji kuwajia juu wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam akiwataka kuacha kumshambulia waziri huyo badala yake wahangaike kutatua matatizo ya msingi ya wananchi katika majimbo yao.
Alisema wabunge hawapaswi kupinga kila jambo kwa lengo la kujijenga kisiasa na kusisitiza kuwa, Waziri huyo ana hoja za msingi, hivyo aungwe mkono kwa lengo la kuboresha usafiri wa majini katika eneo hilo na jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.
“Jamani, ongezeko la Sh100 linaleta chokochoko za nini? Leo hii hata ombaomba ukimpa Sh100 anaweza kukurushia usoni, nadhani wabunge wa Dar es Salaam walipaswa kuunga mkono kwa dhamira kuwa, kivuko kijiendeshe na kutoa huduma za kudumu, badala ya kila kitu kutegemea kitoke Serikali ku.
Mtetezi mwingine ni mkazi wa Makoka, Dar es Salaam, Vicent Michael ambaye amehoji mantiki ya wabunge hao kulalamikia nyongeza ya Sh100 kwenye Kivuko cha Kigamboni wakati wenyewe walisherehekea nyongeza ya Sh200,000 kwenye posho zao za vikao vya Bunge.
“hivi ni kutufanya sisi (wananchi) wapumbavu au vipi? Ni nani asiyejua kama huu ni unafiki. Inaingiaje akilini kuona mtu anasherehekea nyongeza ya Sh200,000 halafu anaandamana kupinga ongezeko la Sh100 kwenye huduma ya umma?”
Najiuliza swali moja, umesoma ongezeko lote na barua yote ya mbunge wa kigamboni au ni wewe ndo shabiki?
ReplyDelete1. kama raia kila mtu ana haki ya kuwa na mawazo tofauti na mwingine, naheshimu yako. Tambua na ya wengine sio wote wanaopinga ni wanasiasa.
2.Hivi umeona ongezeko kwa wenye maguta,mikokoteni na bajaji? naamini umeona nalo unalitetea, guta ni bei juu kuliko gari...... toba yarabi tunusuru viumbe wako.
3. Namba ya miaka si hoja, si dhambi hata bei ikikaa miaka 200 labda sababu kupanda gharama za vitu lakini miaka kama miaka.............sioni hoja hapo.
4. Watu wanalalamika wizi wa mapato feli, magufuli amekubali hilo akasema wataweka mfumo wa kudhibiti, sasa nauli inapanda wakati mfumo wa kudhibiti bado ili ziibiwe vizuri? tunatoka nyuma kwenda mbele au mbele kwenda nyuma? mimi nlijua tunadhibiti ndo tunaongeza!!!!!!yetu mapya twawaongezea ulaji afu tutadhibiti...
Hayo tu kaka, nipatie majibu mimi nsiye mwanasiasa.
Ndugu Anonymous
ReplyDeleteAsante kwa mchango wako mzuri, lakini kwa upande wangu nafikiri jambo ambalo labda Waziri aliteleza ni hilo la kuwakejeli wakazi wa Kigamboni, lakini siku zote anayemalizia ndiye anayeonekena. Wachokozi wametulia;
Pamoja na nukuu nzuri za Mbunge Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile za vipengele kadhaa vya sheria alivyobahatika kuviona lakini binafsi sishawishiki kabisa kuamini Waziri Mhe. Dkt.John Magufuli na jopo lake hawakufanya utafiti kabla ya kuchukua maamuzi. Kwa kauli ya Waziri mwenyewe, hakuna kipengele cha Sheria katika majukumu yake kinachiomtaka aruhusiwe na SUMATRA kufanya mabadiliko kama hayo yayoyafanywa. Sijapata bahati ya kusoma miongozo inayomuongoza Waziri lakini naamini Waziri hawezi kutamka hivyo mbele ya vyombo vya habari na watanzania kama si sahihi katika nyakati hizi ambapo kila taarifa inaweza kupatikana na ikawa wazi kwa jamii.
“a. Guta toka Tsh 200 hadi Tsh 1800 (Asilimia 800); bei ambayo ni kubwa kuliko ya gari ndogo.
b. Bajaj zimepanda toka Tsh 300 hadi Tsh 1300 (asilimia 333).
c. Mikokoteni imeongezeka toka Tsh 200 hadi Tsh 1500 (Asilimia 650).
Isitoshe mizigo inayopakiwa nayo inatozwa nauli.
Wafanyabiashara wengi wa Kigamboni wanatumia maguta, Bajaj na mikokoteni kusafirisha bidhaa.
Kutokana na ongezeko la nauli ya kivuko bei ya bidhaa zimepanda maradufu.
Hali ambayo inazidi kuwatia umaskini wananchi wa eneo hili.”
Lakini Sisi watanzania tumekuwa watu wa kulalamika zaidi kuliko kujua wajibu wetu ni nini na wanasiasa wamekuwa watu wa ku-take advantage ya matukio kujenga majina yao kuliko kutekeleza wajibu wao wa msingi. Hebu fikria ikifika saa 12 jioni hakuna gari itakayokwenda Mbande ndani ya jimbo la Dr. Faustine Ndugulile bila sh. 500, sijawahi kusikia hatua alizochukua, nauli za dala dala zimepanda mara ngapi, bei ya vyakula imepanda mara ngapi, sasa hivi bei ya mchele unakwenda sambamba na sukari, unga utadhani tunaagiza kutoka Marekani, Ubunga Bus Terminal kuingia sh. 200 na hakuna mafuta wala wala mashine inyochakaa kwa kitendo cha wananchi kuingia mle ndani. Kama mishahara, usafi, uedneshaji na maboresho mengine ada zinazolipwa na utitiri wa mbasi naamini zinatosha na fedha nyingine kwa maendeleo zinabaki, lakini watanzania hatujamdhalilisha kiongozi yeyote kwa hayo lakini leo tunaona fahari kumdhalilisha Mhe. Dr. John Magufuli.
Mbunge anasema katika barua yake..namnukuu;
“Aidha, wananchi wa Kigamboni wametiwa simanzi na kuongezewa machungu na kitendo cha tarehe 01.01.2012 kilichofanywa na Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa John Pombe Magufuli (MB) cha kuwatukana na kuwadhalilisha.
Wananchi wa Kigamboni wanamtaka Waziri huyu awaombe radhi. Naomba umshauri Waziri Magufuli afanye hivyo. Ni jambo la kiustaarabu na kiungwana na litalinda heshima ya Serikali”.
Mbunge hajaweka wazi ni nini wananchi wametaka kwa kitendo chao cha kumdhalilisha kiongozi wa nchi mbele ya uma wa watu. Lakini Pia mbunge hajaweka wazi kuwa amewahauri nini wananchi kwa kitendo chao cha kumdhalilisha.
Kuhusu wizi na ubadhirifu ndugu yangu si jambo la busara kuacha kupanga mipango ya maendeleo kusubiri ubadhirifu itokomezwe, hakuna mahali palipo salama nchi nzima, asilimia kubwa ya walalamikaji wanashiriki ubadhirifu katika kuhujumu maeneo ya shughuli zao na kibaya zaidi watanzania wengi wanazihujumu familia zao kwa kufanya ubadhirifu katika fedha wanazozipata kwa mambo yasiyo na manufaa kwa familia zao.