JESHI LA MAREKANI LINATISHA!,
LINA NDEGE ZISIZOPUNGUA 14,500
B-52 ikiwa angani
Manoari ya kijeshi ya marekani yenye uwanja wa ndege za kivita
ikiwa imebeba ndege kadhaa za kivita
Jambo moja ambalo watanzania na watu wengi duniani hawafahamu ni uwezo wa jeshi la anga wa Marekani. Ingawa Siri kamili ya uwezo wa jeshi hilo wanayo wenyewe lakini kwa taarifa ambazo zimefanikiwa kupatikana katika mitandao mbali mbali ya internet ukiwepo mtandao mkubwa wa wikipedia nguvu za jeshi la marekani zinatisha.
Taarifa katika mitandao zinaonyesha kuwa jeshi la anga la Marekani linamiliki ndege zisizopungua 14,500 zinazofanya kazi. Idadi hii ya ndege ni kubwa na huenda hakuna nchi duniani ambayo inaweza kufikia idadi za ndege za jeshi hilo. Aidha wakati urusi ikitajwa kumiliki silaha nyingi sana za kivita mitandao haijawa na kumbu kumbu za uhakikika wa hali za zana ambazo Urusi hadi hivi sasa inazo.
Katika ndege hizo, Marekani inamiliki ndege 74 aina ya B52 ndege zenye enjini nane, ni ndege ambazo ndizo ndege kubwa zaidi duniani katika historia ya ndege za kivita. Ndege hizo ambazo kubwa kuliko ndege zote za kivita duniani ambazo pia ni muundo ambao haziwezi kudondoshwa kirahisi ni maalumu kwa mashambulizi mazito yakiwemo mashambulizi ya mabomu ya nyuklia.
Aidha katika idadi hiyo ya ndege inazomilikiwa ndege 174 zimetengenezwa kuwa ushirkiano wa Marekani na kanada, 118 Uingereza na Marekani, 13 Marekani na Italia. Ndege 20 ni za kirusi, Ndege 142 ni za Kifaransa, ndege 43 ni za kiingereza, 23 za kikanada, 4 za Poland, 2 za Kiholanzi, 13 za kihispania, 2 za kiswitzerland. Ndege nyingine zimetengenezwa na marekani wenyewe na baadhi ambazo idadi yake haijafahamika zimetengenezwa Israel.
Dhu...!! america inatisha
ReplyDelete