Thursday, April 19, 2012

FURAHA ILIMUUA STEVEN KANUMBA "THE GREAT"?

Steven Kanumba akifurahia moja ya tuzo alizopata
nchini Marekani Mwaka 2008 (Picha na Mrisho's Blog)

Inaelezwa kwamba masaa takriban 10 kabla ya kifo chake aliyekuwa muigizaji maarufu zaidi nchini Tanzania Marehemu Steven Kanumba "The Great" alikuwa amesaini mkataba mkubwa sana na Hollywood ya nchini Marekani. Inaelezwa kwamba mkataba huu ungemfanya awe mbali na Tanzania kwa muda mrefu na kuwa bilionea.

Wakati watu wengine wakidekeza hisia zao na kuhisi zababu za kifo cha Kanumba kurogwa, sumu nk  nikizidekeza hisi zangu na mimi inawezekana kabisa sababu za kifo cha kanumba zilianzia kwenye furaha kubwa aliyokuwanayo siku hiyo baada ya kusaini mkataba huo mzito.

Inawezekana kabisa Kanumba alikuwa hajiamini kwa kupata mkataba huo na baadaye kulipuka kwa furaha iliyopitiliza ingawa ilikuwa zaidi ndani ya moyo wake. Na kutokana na furaha hiyo inawezekana aliamua kunywa pombe na kujikuta akipitiliza kiwango ambacho huwa anakunwa. Aidha nyakati za usiku aliamua kutoka na mdogo wake na inawezekana pamoja na msichana anayempenda sana Elizabeth Michael "Lulu". 

Kwa utafiti wangu binafsi mtu anapokunywa pombe kasi ya mzunguko wa damu mwilini huwa ni kubwa. Na mtu anapopatwa na mshituko ama hasira na jazba mapigo ya moyo pia huongeza kasi na kuongeza msukumo wa damu mwilini.

Kuna uwezekano mkubwa ikiwa alikunywa pombe kali mzunguko wa damu ulikuwa mkubwa na kasi ya mzunguko huo liongezeka ghafla kutokana na mshituko na jazba zilizotokana na Lulu kupokea simu. Kutokana na hili kuna uwezekano mkubwa mishipa ya Damu katika Ubongo ilizidiwa ghafla na kupasuka sehemu fulani ambayo Madaktari hawakuweza kugundua mara moja kutokana na teknolojia duni tulizonazo.

Steven Kanumba Siku ya Sherehe yake ya Mwisho 10.4.2012
R.I.P Kanumba

Aidha na kwa walichokiona madaktari inawezekana pia kutokana na pombe na hasira ilikuwa rahisi sana kwake kuyumba na kujigonga kwa nyumba ukutani kiasi ubongo ukatikisika wakati binti mdogo Lulu alipokuwa akijaribu kujiweka salama na hasira alizokuwa akiziona.

6 comments:

  1. nasikitika sana na habari hii hata nashindwa kuandika yaliyomo moyoni..R.I.P kanumba

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli hatujui ni mkataba mkubwa ama vipi lakini kile kitendo cha kuigiza mambo mengi ya kimungu mengi kati ya movie zake nyingi yananifanya ninatamani kwamba kijana wetu angekufa kifo cha kitakatifu chenye kutujulisha kwamba ameenda mbinguni kwa baba jamani -lakini hivi ilivyotokea naogopa ,nasikitika na sijui -dakika za mwisho anaweza kuwa alipata wakati wa kuongea na mungu -hiyo siri anajua Mungu kweli mimi siwezi kuhukumu mimi ni mnyonge binadamu nisiyejua. ila ninaomba tu tujifunze somo la uinjilisti ambalo bado ametufundisha hata katika mauti yake kwamba duniani ,mali utajiri, heshima nakila kitu ni bure tu -unapopata mali unaongeza ubatili , maadui wanaongezeka , wanafiki wanakufuata , wewe mwenyewe unawezakuchanganyikiwa , na shetani naye anaangaliaga hapo hapo!! yaani duniani ni ubatili mtupu na kujilisha upepo -kweli ndugu zangu tumkilimbilie Yesu atosha

    ReplyDelete
  3. no coments rest in peace steven kanumba the great

    ReplyDelete
  4. Ni kweli msemayo .. kifo cha Kanumba kimisikitisha wengi .. mimi sikuwa mpenzi sana wa Bongo movies lakini kifo hicho kilinishitua .. kwani jamaa kazi zake nyingi zilikuwa na mafunzo muhimu kwa jamii.. la msingi hapa tunapaswa kujifunza maana kifo cha Kanumba kimefunua mambo mengi yaliyokuwepo nyuma ya pazia ingawa mengine hayajathibitishwa. La msingi hapa ni kujifunza .. wasanii wajifunze, na jamii kwa ujumla tujifunze.

    ReplyDelete
  5. Tunahitaji sana kumtegemea Mungu maana uhai tuliyonao upo mikononi mwake, Kifo cha kanumba kimenisikitisha sana kama mdogo wangu, nilikuwa napenda movie zake alikuwa anatumia hisia sana msg tulikwa tunapata either kufundisha au kuonya. Kikubwa ni kukaa katika kumtegemea Mungu peke yake na kwa vijana tuwe na muda wa kumtafuta Mungu na siyo kuweka starehe mbele maana hatujui siku wala saa.

    Neno la Mungu linasema alaaniwe anaye mtegemea mwanadamu na vitu vyote vyenye thamani, fedha na dhahabu ni mali yake, kwahiyo akitubariki lazima turudi mbele zake kwa shukurani maana mungu anasema anapendezwa na moyo wa shukrani. utajiri usitutenge na uso na Mungu.

    kanumba ameondoka wakati wa kufanikiwa sana na sisi tukague njia zetu ili wakati tusioujua tuwe tayari maana hakuna jina kuu mbinguni na duniani zaidi ya Mungu.

    Mama Kanumba anahitaji kuombewa sana ili Mungu amtie nguvu na kama mzazi ameumia sana, Mungu akupiganie, akutetee na akushindie kwenye hiki kipindi.

    Amen

    ReplyDelete
  6. It's realy paining when someone u love become a memory.The memory become a treasure forever. W'LL MIC EVER AND U W'LL BE THE REMENDER IN OUR BRAIN. R.I.P. BROTHER.

    ReplyDelete