Saturday, May 1, 2010
WASIOONA TEMEKE WAPATA MAFUNZO YA UTAWALA BORA
Katibu wa TLB Temeke, Bw. Jega akisoma risala
Mmoja wa Washiriki, Bw. Madebe akipokea Cheti, kulia ni Mwezeshaji katika Mafunzo hayo.
Picha ya pamoja washiriki wote, mwezeshaji, wahudumu na Mgeni Rasmi, waliokaa wa pili kutoka kushoto ni Mweka hazina wa TLB Temeke Bw. Mussa Njechele
VIONGOZI wa Chama Cha Wasioona Wilaya ya Temeke (Tanzania League of the Blind wamepata mafunzo ya Uongozi na Utawala Bora ili kuboresha ufanisi katika kukiendesha Chama Chao Wilayani humo.
Mafunzo hayo ambayo yalikuwa ni ya siku nne, yalifanyika Jijini Dar es salaam kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la Foundation for Civil Society (FCS) lenye makao yake makuu jijini Dare s Salaam.
Mafunzo hayo ambayo yalikuwa ni ya siku nne yalianza Tarehe 26 April na kufikia tamati tarehe 29 April yakiwa yameshirikisha wasioona wapatao 25 ambao ni viongozi wa ngazi ya Wilaya na Matawi yote yaliyopo katika Wilayani ya Temeke.
Akisoma Risala ya Chama hicho kwa mgeni Rasmi Mbunge wa jimbo la Temeke Mhe. Abasi Mtemvu, ambaye aliwakilishwa na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Majimatitu mahali ambapo mafunzo hayo yalifanyika, Katibu wa Chama hicho Bw. Seif Jega alisema mafunzo hayo yatawasaidia sana kuinua ufanisi katika Chama Chao na kwamba cham hicho kinawashukuru sana wafadhili waliowezesha kufanyika kwa mafunzo hayo muhimu.
Aidha alisema chama hicho kina wanachama 200 lakini wasioona Wilayani humo ni zaidi ya mia mbili ambao wanahitaji kufikiwa na kwamba chama hicho kina matatizo mengi ikiwemo tatizo la kutokuwa na ofisi ya kudumu kwani sasa wamehifadhiwa na mtu mwenye mapenzi mema na wasiona. Aidha alisema pia wana matatizo ya fimbo kwa wanachama wao wengi, usafiri kwa shughuli za kiofisi na vitendea kazi vya ofisini.
Wasioona hao wamewaomba wasamaria wema kujitokeza kuwasadia ili kupata mahitaji muhimu yatakayowawezesha nao kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa, kwani uwezo wa kushiriki kuleta maendeleo ya nchi wanao endapo watawezeshwa.
Kushoto ni mwenyekiti wa TLB Wilaya ya Temeke, Bw. Abdalla Sauleni, Katikati ni Katibu Bw. Khamisi Seif Jega na kulia ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo bw. Jacob Malihoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ukiwapa nafasi wanaweza.
ReplyDeletewasioona wanaona tusivyoweza kuona siye wenye macho!! :-(
Chacha! we acha tu hawa jamaa wana akili za ajabu sasa, na uwezo wao unashangaza. Nimejifunza mengi sana katika mafunzo haya niliyokuwa nikiwafanyia. Siku chache zijazo nitakuja na kazi na ujuzi wa baadhi yao..utashangaa! ili niliumizwa na jambo moja.. hawa jamaa hawana ofisi..walialika wafanyabiashara, wanasiasa, na viongozi waje siku ya kufunga mafunzo labda risala yao atajitokeza mtu awasaidia.. kilichotokea ni kwamba wamejikuta wako wao, mwezeshaji wao na Mjumbe wa serikali ya mtaa, ambaye aliamua kuchukua nafasi ya Mgeni Rasmi!
ReplyDeleteSafi sana hii nimeipenda kwa kweli.
ReplyDelete