Baada ya kuwa bize kwa muda wa miezi 6 hivi, ninarudi tena mtandaoni. Nilipotea ghafla lakini mliotembelea kibalaza hiki mnaweza kujua ni kwa nini nilipotea kwa muda.
Hata hivyo pamoja na heka heka ambazo sikufanikiwa nimekuwa na majukumu mengine kadhaa yanayoninyima muda wa kutosha kublog. Kuna wakati nililazimika kujifungia chumani, kuna wakati nililazimika kupandisha vioo vya gari mpka juu nisisikia sauti yoyote, rafiki waliojaribu kunipigia kelele sikusikia..wote waliokerwa wanisamehe tafdhali.. nilitingwa mno..tena mno.
bado bado kidogo lakini nitaanza kupata muda wa kupunga upepo wiki chache zijazo, mtaanza kuniona hewani, ingawa si kwa mfululizo kama walivyo blogers wengine.
STAY TUNED FOR MORE HAPPY DAYS!
Ama kweli ulipotea mno mpaka tulianza kukusahau. Pole kwa malengo yako kutokwenda sambamba. Ila tunafurahi upo nasi tena Mungu mkubwa ipo siku itakuwa siku yako na wala usikate tamaa. Karibu sana tena!!
ReplyDeleteNashukuru kwa hisia zako nzuri kwa kukwamba kwangu. Lakini binafsi nawasikitikia na kuwapa pole ndugu zangu wa Jimbo la peramiho. kimsingi utakatifu uliniponza... hebu cheki jambo la ajabu .. kuna mahali niliwaeleza wananchi hivi "ndugu zangu kina mama, kina baba, na vijana wenzngu .. vitu vidogo vidogo tunavyopata sasa ni sawa na pipi, ambayo hunoga kwa muda mfupi na kisha njaa kubaki palepale" wabibi waliovaa sare wakaguna.
ReplyDeleteNiligundua jambo .. nikawahurumia sana na mchungu makali yalinipata!
Lakini nimejifunza mengi sana .. na kwa namna moja au zaidi nashukuru..kwa kushindwa kwangu wengi watapona! asomaye na afahamu!
Lakini ningeshinda labda nisingepata machungu ambayo yamekuwa yakiliathiri taifa katika maeneo mengi.
usikate tamaa ya kupenda kutumikia watu wako,hao watoa rushwa siku yao itafika na watu haohao anaowapa pipi wataamka.
ReplyDelete