Tuesday, November 30, 2010

Mapotopoto Kuuzwa Dar Karibuni

Mapotopoto "Masuku" Kuuzwa Dar Karibuni

Vikapu na Ndoo hutumika kubebea Masuku

Kina mama wakiuza Masuku katika viunga vya Misheni ya Peramiho, Songea
Mkoani Ruvuma kama walivyokutwa na mwandishi wa makala hii- Jacob Malihoja

Picha Mbili zilizofuatana; mteja Jacob Malihoja akijifaidia matunda ya mapotopoto "Masuku" baada ya kununu kutoka kwa akina mama hao
NB: Picha zote zilipigwa Mwishoni mwa mwaka 2008
na Jacob Malihoja,

Makala yangu ya “Mapotopoto: matunda pori yenye sifa tatu:” kwa mara ya kwanza ilitumika katika gazeti la Mwananchi mapema Februari 2009, Mwanachama mmoja wa mtandao wa JamiiForums ajulikanae kwa jina la MziziMkavu akairusha kwenye mtandao huo na kisha mwaka mmoja baadae, dada Yasinta Ngonyani baada ya mawasiliano yangu nae kumkumbusha matunda hayo Jumatano ya Februari 3, 2010 akairusha kwenye blog yake. Nilifurahi sana kwa kuwa blog yake ina wasomaji wengi.

Wanablog wakachangia, wengi walionyesha kutoyafahamu matunda haya ya asili, ambayo kimsingi hamna anayehangaika kuotesha miti yake..

Dada Lulu yeye alipendekeza Yasinta atafute picha, hoja iliyoungwa mkono na blogers wengine. Bwana Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! Aliuliza; “Yasinta: yakiiva yana rangi gani na yakiwa machanga yanakuwaje? yana utomvu?”


Matunda haya yakiwa katika hali ya ubichi, hayaja komaa ila yanaelekea kukomaa Picha: kwa Hisani ya Blog ya Ruhuwiko

Dada Koero Mkundi nae hakubaki nyuma, alifananisha matunda haya na matunda aliyoyazoea kule upareni na kuuliza “Siju ndio yale tunayoyaita matopetope kule upareni?”


Simon Kitururu yeye amewahi kuishi mkoani Ruvuma, lakini hakuyakumbuka kabisa matunda haya maarufu, yeye akasema “Hapa picha ingekuwa Msaada sana. Ingawa nimewahi kuishi Ruvuma, Songea nilikosomea shule ya vidudu na kuanza shule ya Msingi Mfaranyaki] Sina kumbukumbu Mapotopoto ndio nini.:-(.”


Nahisi Kitururu alisoma kule kwa muda, au geti lilikuwa kali sana asile vitu asivyovijua, ahaa! Nimekumbuk!a miaka ya zamani matunda haya yalikuwa sio dili .. inawezekana ndio maana kwasababu alikuwa mjini hukuyaona.


Kwakweli nilifurahi na michango .. na maswali kutoka kwa blogers .. jambo ambalo linanipa picha na kusogea zaidi kutambua kuwa idadi kubwa ya Watanzania wasiotoka maeneo yale yanakopatikana hawayajui na kwamba wanakosa uhondo mkubwa.


Kwa ufupi matunda haya kwa mkoa wa Ruvuma ni maarufu kwa jina la Mapotopoto, lakini vile vile hufahamika sana kwa jina la Masuku, nan baada ya utafiti wangu Watu wengi wanaamini hilo ndilo jina la matunda hayo kwa kiswahili. Matunda haya pia yanapatikana mkoa wa Iringa ambapo maeneo mengi katika mkoa huo yanajulikana kwa jina la Makusu, hali kadhalika nimeelezwa kuwa yanapatikana Mkoa wa Rukwa na Mbeya ambako huko hujulikana kwa jina la Masuku.


Kwa sasa najaribu kuona ni jinsi gani matunda haya ya msimu yanaweza kuingia katika soko, jambo ambalo naamini likiwezekana litakuwa na faida takribani nne, Kwanza watanzania wengi nzaidi watapata kuyajua na kuyala matunda haya, faida ya pili itasaidia kutengeneza kipato kwa wananchi yanakopatikana, tatu kwakuwa yatakuwa dili miti yake italindwa na hatimaye mazingira yatasalimika na tatu inaelezwa kuwa takataka za matunda hayo (maozea yake) ni mbolea tosha ya zao la uyoga hususani ule wa asili. Na faida nyingine kadhaa zinaweza kupatikana.


Na huu ndio mzimu wa matunda haya katika maeneo yanakopatikana. Aidha waklati wowote kuanzia mwisho wa wiki hii matunda haya yatakuwepo katika soko la utafiti jijini Dar Es Salam, kwani nimeagiza kiasi fulani kwa ajili ya kazi hiyo.

3 comments:

  1. Nimefurahi umeiibua hii mada tena kwa kweli unafanya vizuri kabisa kama ulivyosema ni matunda ambayo yameoteshwa na mungu mwenyewe. Nilipoangalia picha hizo na humu kwenye kikapu (kidengu) nimetamani kweli je unaweza kufanya utafiti wa matunda ya "madonga pia"?

    ReplyDelete
  2. Asante kwa ushauri, Yasinta. Ninakuahidi kuwa endapo mkakati wangu wa utafiti wa Masuku ukifanikiwa hatua yangu ya pili itakuwa ya utafiti kuhusu MADONGA (Matonga).

    Lakini vile vile nitafanya utafiti mwingine kuhusu mabuni na Mangatungu na aina nyingine mbali mbali ya vyakula na matunda mazuri yanayopatikana Songea ambayo wakazi wengi wa miji mingine hawayajui.

    Lakini vile vile ningependa kuona watanzania wenye taarifa nyingi zaidi ya matunda na vyakula vya asili kuviweka hadharani ili vieleweke na jamii ya kitanzania ifaidike navyo.

    ReplyDelete
  3. kwa kweli ni moja kati ya matunda ninayoyapenda kuliko mengine yote!!!! nimefurahi sana kuyaona "mapotopoto" ni matamu... na sukari yake lalalalalaaaaa..... usitake onaaaaa!!!!

    ReplyDelete