Thursday, November 4, 2010

“MPENZI WA KWELI”


KITABU CHA MAADILI YA WANAFUNZI

“MPENZI WA KWELI”

Baada ya uchunguzi wa kina nilioufanya kwa muda mrefu, nimegundua mambo mengi yanawakwamisha vijana kusonga mbele kufikia ndoto zao kielimu na kimaisha. Vijana katika masomo wanakumbana na changamoto kubwa sana ya mahusiano ya kimapenzi na tamaa ya vitu ama mambo ya kisasa.


Jamii, asasi mbali mbali na Serikali zimekuwa zikitumia mamilioni ya fedha kukabiliabna na adui wa vijana ambaye ukimtazama kwa asilimia ni kama hayupo na kuacha adui mkuu wa kijana ambaye ni akili yake kijana mwenye.


Kumekuwa na juhudu kubwa za kukabiliana na wanaodaiwa mijibaba na miji mama kuchukua wasichana wanafunzi “wadogo” ama wavulana wadogo. Lakini ukweli ni kwamba hakuna msichana hata mmoja mdogo au mvulana hata mmoja mdogo ambaye anaweza kuwa tayari kuchukuliwa na mtu mzima kama hajawahi kufanya mchezo huo na mvulana wa umri wake au mwenye umri unaokaribiana sana. Hali kdhalika hakuna mvulana anayeweza kuwa tayari kwenda na mwanamke mtu mzima kama mvulana huyo hajawahi kujaribu mambo hayo na msichana wanayekaribiana umri. Kwa msichana asiyewahi kufanya tendo hilo, kwa mtu mzima atafanya kwa kubakwa matukio ambayo ni asilimia 0.00000000001 katika jamii.


Matukio mengi ya watoto kujiingiza katika mahusiano yanaanza kwa kuharibiana wenyewe wa umri unaofanana kabla ya kuanza kujihusisha na watu waliowazidi sana umri.


Kitabu cha mpenzi wa kweli ni kitabu kinachoshughulika na adui wa kijana ambaye ni akili yake mwenyewe, ni kitabu ambacho kinaelezea changamoto nyingi anazokumbana nazo kijana hususani mwanafunzi nan hatari iliyopo mbele yake na namna ya kyukabiliana nayo. Ni kitabu ambacho lengo lake ni kumfanya kijana ajitambue na kuchukua hatua muhimu kwa maisha yake. Kitabu hiki kina nguvu ya ajabu.


Mwalimu Abasi wa shule ya Sekondari ya Kent alijiwekea utaratibu wa kuwasomea wanafunzi wake kabla para chache kabla hajaanza somo, na wakati mwingine alimwita mwanafunzi mmoja awasomee wenzake, kisha akawapa maelezo mafupi ya ziada. Mwanafunzi Ibrahim wa Shule hiyo ya kent ambaye alinipa habari hiyo, alinieleza jinsi kitabu hicho kilivyosambaratisha makundi ya ujinga na upuuzi katika darasa lao mpaka walipomaliza mitihani yao ya kidato cha nne. Anasema kitabu hicho kiliwabadili mwelekeo kwa namna ambayo hajawahi kuona… akaongeza kwa kusema laiti kama wangeanza kukisoma tangu wapo kidato cha tatu mambo yao yangekuwa mazuri kupita kiasi.


Unaweza kuwasiliana nami kwa njia ya simu ama barua pepe

Email: malihoja@yahoo.com

Simu: 0716 909171 na 0756 680 200

1 comment:

  1. Ahsante kwa mwonjo wa kitabu cha MPENZI WA KWELI, kinaonekana ni kitabu chenye mafunzo mazuri sana.

    ReplyDelete