Wednesday, July 25, 2012

Vyombo vya Habari Vinanishangaza

Vyombo vya habari Tanzania vinanishangaza!

  HONGERA NDITI

Adam Nditi
Kijina wa Tanzania aliyesajiliwa na Chelsea hivi karibuni, Mungu Mbariki Adamb Nditi afanya makubwa na kuipaisha Tanzania, Mungu Ibariki Tanzania iendelee kupata namba timu kubwa za Ulaya.

= = =

Adam Nditi

Born 18/9/94 in Zanzibar, Tanzania.Adam arrived at Chelsea as an Under-13 and can play either left-back or left-wing. It was the more defensive of those roles he filled as the FA Youth Cup was captured in 2012. He was joint-highest youth league appearance maker and played four games for the reserves in 2011/12, his first full-time season which led to a professional contract.
As a schoolboy he amassed 27 youth team appearances, and featured regularly during the 2011 FA Youth Cup run.to the semi-final.
Very quick, he bases his game on Ashley Cole, and enjoys taking players on. 

http://www.chelseafc.com/page/AcademyProfiles/0,,10268~1333485,00.html

= = = = =



Footballzz.com

http://www.footballzz.com/jogador.php?id=178506&epoca_id=0&search=1

 
Moja ya mafanikio makubwa mabayo Tanzania imeyapata duniani ni kupata namba katika timu kubwa sana duniani. Maelfu kwa Malaki ya vijana wenye vipaji kutoka nchi mbali mbali Duniani wamekosa nafasi hiyo, na maelfu kwa malaki wanapambana kupata nafasi hiyo. Kitendo cha Adam Nditi kupata namba Chelsea ni hatua ambayo ilipaswa kupokelewa kwa shangwe na Watanzania wote. Nilitarajia kuona magazeti ya Tanzania yanakuja na Lead Story Front Page juu ya hili ikiambatana na Picha kubwa. Lakini ni tofauti kabisa, waandishi wazalendo wachache ndio naona wanaandika andika habari za huyo dogo. Inaniuma, inanishangaza na kujiuliza uzalendo uko wapi .. kelele za vyombo vya habari kutaka maendeleo ya soka zinaishia kulaumu tu wala sio kusifia na kuhamasisha mafanikio yanapoonekana. Au wivuu au nini? .. Watanzania wengi wa kawaida hawana habari juu ya mafanikio haya makubwa tuliyoyapata. Ingekuwa nchi za wenzetu tayari vyombo vya habari vimeshamfuata na kufanya mahojiano naye na kumtia Moyo. Natoa rai kwa rais kikwete Kumtumia salamu za pongezi kijana huyo, kumtia moyo na kumfanya ajue kuwa Taifa lipo nyuma yake, asifanye mchezo.

1 comment: