Tuesday, August 7, 2012

CONGRATULATIONS AMERICA

HONGERA MAREKANI,

KWA KUFIKISHA CHOMBO MARS!

MUNGU IBARIKI MAREKANI!

======
Kuna Watu wanaitazama na kuisema Vibaya Marekani na wengine hufurahi Marekani inapofanyiwa hujuma nzito. Kihistoria miaka ya nyuma hakuna Taifa ambalo sisi waafrika tunaweza kusema lilikuwa jema kwetu, Si Ulaya, Si Marekani wala si Arabuni hao wote walikuwa wabaya kwetu, kila mmoja kwa namna yake. Marekani ingekuwa Mbaya hata wanaoiponda wasingetamani kwenda huko! Lakini leo hii hao hao wanaoiponda na kufurahi inapohujumiwa wenyewe wanatamani kwenda Marekani. Sijui tuwaiteje hao!
========
Binafsi Marekani ni nchi yangu ya tatu kuuipenda, Ya kwanza Tanzania, ya pili Uholanzi na ya tatu ni Marekani. Naipeda America na naitakia baraka na mafanikio zaidi kiuchumi, kisayansi na kijamii.
Marekani ina mchango mkubwa sana katika maisha na maendeleo yangu pamoja na wewe msomaji wa mada hii. Baada ya Mwingereza kugundua mafuta, Marekani ndio wamekuwa wa Kwanza Kuchimba Mafuta duniani pale Penislevania, Aidha pamoja na juhudi nyingi kufanyika katika nchi mbali mbali Redio, Bulb za umeme, Computer, Internet, Email, Simu, telefax na vitu kadha wa kadha vimegunduliwa Marekani na vingine kuboreshwa na kuendelezwa Marekani, leo hii dunia imekuwa kijiji.
========
Marekani ndiyo iliyokomesha kampeni ya Wajapani kuwaua Wachina kwa Halaiki. Marekani ndiyo iliyokomesha kampeni ya Hitler kuwaua Wapolland, Waholanzi, Waisrael nk.kwa halaiki nk.

Bila Marekani leo hii Urusi ingekuwa inaendelea kuikalia Afganistan. Bila Marekani leo hii huenda Korea ya Kaskazini ingeshaivamia Korea ya Kusini. Bila Marekani huenda India na Pakistani zingeshatwangana. Bila Marekani huenda China ingeshaishambulia Taiwan, Bila Marekani huenda China ingeanshisha Vita na Japan. bila Marekani leo hii Irani ingeshaivamia Israel.
=========
Ingawa kwa leo hatua zinazochukuliwa na Marekani katika migogoro mingi zinachukiwa na baadhi ya watu lakini ukweli ulio wazi bila taifa lenye nguvu kijeshi, kiteknolojia na Sera kama Marekani basi hii dunia kwa sasa pangekuwa hapatoshi.


MUNGU IBARIKI MAREKANI!

2 comments:

  1. nakupongeza kaka kwa kazi nzur.
    Kwa upande wangu Taifa ninalolipenda ni Israel, alafu Marekani.
    Nimevutiwa xana na makala ambazo umekuwa ukiziandika kuhusu mataifa haya mawili.
    MUNGU AKUBARIKI SANA.

    ReplyDelete
  2. Vilevile unaweza kunitumia makala au hata links ambazo zitanipatia habari zaidi juu ya Mataifa haya.
    Email yangu ni ephraimpeter632@gmail.com

    ReplyDelete