MAUMIVU
MAKALI YA MGUU, MGONGO, BEGA AU MKONO.
SPINAL DISC (DISC ZA UTI WA MGONGO)
ZINAVYOLETA MAJANGA
Spinal
Disc ni disk zinazokaa kati kati ya pingili “Spinal Vertebrae” za uti wa mgongo.
Kuna wakati disk hizo hutoka sehemu yake na kusogea pembeni tatizo ambalo linajulikana
kwa majina kadhaa kama vile DEGENERATIVE DISC DISEASE au HERNIATED DISC au SLIPPED DISC. Tatizo hili husababisha maumivu
makali ya mguu, mgongo, bega au Mkono. Maumivu haya huwa ni makali mno, katika
mazingira mengine huuja na kutoweka, katika mazingira mengine maumivu haya huwa
endelevu.
Naamini
wengi wetu tumeshawahi kusikia au kuona ndugu, rafiki, jamaa, jirani fulani
akiumwa mguu, mkono, bega au mgongo tena kwa maumivu makali sana.
Wengi
wamehangaika hospitali nyingi bila mafanikio, wengine wamekimbilia kwenye
huduma za maombezi na wengine wamekimbilia kwenye tiba mbadala na wengine
wamekimbilia kwa Sangoma.
Kote
huko wamekosa ufumbuzi wengine wamepoteza maisha na wengine wamepata kupooza
kabisa mguu au miguu wakiwa wameshatuoa fedha nyingi sana na mateso makali.
Nilibahatika
kufanya mazungumzo na baadhi ya waliowahi kupatwa na matatizo kama haya. Ndugu Selemani
Mkoba alinielezea tatizo hilo lilivyomtesa na baada ya kuhangaika hospitali kwa
zaidi ya miezi 3 wakati wote kiteseka kwa maumivu makali na kupoteza hela
nyingi bila mafanikio aliamua kwenda kwa waganga wa kienyeji. Anasema Mganga alimpa
matumaini makubwa lakini wiki kadhaa zikawa zinapita bila kupata unafuu wowote.
Anasema Mgonga alikuwa akimpa matumaini kwa kumwambia ugonjwa unaingia ghafla
lakini kutoka unatoka taratibu sana . Ndugu Mkoba anasema kwa bahati alipomwelezea
tatizo hilo mmoja wa rafiki zake ambaye si daktari alimwambia aondoke haraka huko na kuwahi Muhimbili.
Rafiki yake huyo alimweleza kuwa analifahamu tatizo hilo.
Ndugu
Mkoba amasema alienda Muhimbili kama alivyoshauriwa na rafiki yake, akafanyiwa kipimo cha MRI ambapo waligundua tatizo hilo katika
uti wa mgongo na kupangiwa siku ya upasuaji. Alifanyiwa upasuaji na alipozinduka
alikuwa na maumivu makali ya wastani yatokanayo na upasuaji tu .. maumivu ya
mguu hayakuwepo tena. Maumivu yatokanayo na upasuaji yaliendelea kupungua na
sasa ni miezi mitatu amebakiwa na maumivu madogo sana mbayo yanaendelea
kupoteza huku akiendelea na mazoezi. Anaweza kuendesha Gari, anaweza kutembea na
kufanya shughuli zake ambazo zilisimama. Aidha Ndugu Mkoba anasema angependa
watu wajue hili ili wasi mateso aliyoyapata yeye na walio kwenye mateso hayo wapate
ufumbuzi haraka maana ni mateso yanayotisha.
MGAWANYIKO WA UTI WA MGONGO NA MATOKEO
YA DISCK ZINAPOCHEZA
Uti
wa mgongo umegawanyika katika aina kuu zipatazo nne (4) za pingili “Spinal
Vertebrae”
Cervical Curve: Hili ni eneo la juu la uti wa mgongo, Eneo hili
linaanzia uti wa mgongo unpokutana na kichwa na kuishia eneo la mwisho la
Shingo, kwa lugha nyepesi ndilo eneo linalomiliki shingo, pingili zilizopo
katika eneo hili zinaitwa “Cervical Vertebrae”.
·
Maeneo
yanayoathiriwa na Disc kucheza katika eneo hili “Cervical Disc Herniation” ni Mikono au Mabega au kifua, moja wapo
ya viungo hivi vitapata maumivu makali sana.
Thoracic Curve: Hili ni eneo la uti wa mgongo linalofuatia kuelekea
chini likianzia inapoishia Shingo, Eneo hili linaishia katikati ya mgongo, kwa
lugha nyepesi eneo hili ndilo linalomilike mbavu. Pingili zinazopatikana katika
eneo hili zinaitwa “Thoracic Vertebrae”.
·
Kucheza kwa disck
katika eneo hili kutakusababishia maumivu makali ya Mgongo eneo la juu ya
Kiuno.
Lumbar Curve: Eneo hili linaanzia inapoishia Thoracic Curve na
kuelekea chini na kukutana na Eneo linaloitwa Sacral Curve au eneo la kiuno
linapoanzia. Eneo la Lumba linazungukwa na ma matumbo na mazagazaga mengine
yasiyokuwa na mifupa. Pingili za uti wa mgongo zinazopatikana katika eneo hili
zinaitwa “Lumbar Vertebrae”
·
Ikiwa Disc
zitacheza katika eneo hili mhusika atapata maumivu makali ya mguu maumivu
ambayo yaukumba mguuu wote kuanzia sehemu ya ndani ya tako na kushuka chini
mpaka mwisho wa mguu kwenye kisigino.
Sacral Curve: Eneo hili linaanzia pale
Lumbar Curve inapoishia hadi mwisho wa uti wa mgongo kwa chini. Katika lugha
nepesi eneo hili ndilo linalomiliki kiuno. Pingili zinazopatikana katika eneo
hili zinaitwa “Sacral Vertebrae”
SABABU ZA MATATIZO HAYA
·
Ajali ya Gari
·
Kuanguka
·
Kupigwa/kupigana
·
Michezo
·
Ajali katika sehemu za kazi
·
Kasoro wakati wa kuzaliwa
·
Kubeba vitu vizito
·
Ukaaji mbaya wa muda mrefu
·
Misukosuku mbali mbali ya mwili kama
MATIBABU
Tatizo
hili linatibika ikiwa mgonjwa atawahi kufanyiwa uchunguzi sahihi na tatizo hilo
kugundulika. Kuna matibabu ya namna tofauuti
ambayo daktari anaweza kukupa lakini hali inapokuwa mbaya Madaktari hulazimika
kufanya upasuaji. Mgonjwa anatakiwa kupimwa kwa vipimo sahihi na kipimo kinachoAMINIWA
zaidi ni MRI. Aidha kwa bahati Tanzania moja ya nchi chache barani Afrika zenye
mitambo hii ya MRI na moja ya nchi chache barani Afrika zenye madaktari bingwa
wa matatizo haya.
Wadau badala ya ya kutumia fedha nyingi kwa waganga
wa kienyeji tuwahi hospitali hususani Muhimbili kuonana na mabingwa wa NEURAL.
Rai yangu kwa serikali pamoja na kuwa sisi tumekuwa moja katika nchi chache
zenye huduma hii, mahitaji ya Madaktari hawa ni makubwa sana bado, Serikali
ipeleke Madaktari zaidi nje kwa ajili ya kupatiwa ujuzi huu na kuongeza mashine
za MRI angalau zifike 10.
NAMNA
YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI
Matunzo
mazuri ya ujauzito
Kuepuka
kipigana au kupigwa, usimpige mwenzako kwasababu unaweza kumsababishia tatizo
baadae
Kama
unaendesha gari ama piki piki kuepuka mwendo unaoweza kukusababishia ajaili
Uangalifu
katika michezo na mazoezi mazito
Kujilinda
kiafya ili kujiepusha na maradhi yasiyotambulika
Tujiepusha
na ukaaji mbaya wa muda mrefu katika sehemu zetu za kazi, pendelea kutafuta
maelekezo jinsi ya kukaa katika sehemu yako ya kazi.
Pendelea
kuangalia afya mara kwa mara na kupata ushauri wa madaktari.
MWISHO
Napenda
kuwajulisha wasomaji wangu kuwa mimi si daktari, sijawahi kupitia fani hiyo
nimeandika makala hii baada ya kupitia uzoefu mbali mbali, kuhoji waliowahi
kupatwa na matatizo haya na kufanya utafiti kupitia mitandao mikubwa ya
kitabibu Duniani, kwa kusoma kazi za madaktari bingwa katika mitandao hiyo. Kwa
namna moja au zaidi inawezekana kuna mahali nimeweka maelezo yasiyo na usahihi
kwa asilimia 100, naomba usiitumia taarifa hii kama sehemu ya matibabu, bali
itumia taaruifa hii kuchukua hatua sahihi.
kaka asnte kwa kujitoa muda wako kwa ajili ya afya zetu,mimi nadhani naweza kuwa mhanga ntajitahidi kufanya hivyo
ReplyDeleteubarikikiwe kwa maelezo mazuri....
ReplyDeleteASANTE KWA MAELEZO MAZURI UBARIKIWE
DeleteInawezekana kupona kama mtu amevunjika uti wa mgongo?
ReplyDeleteNipe jina la doctor bingwa wa tatizo la pingiri ya uti wa mgongo au contacts zake niwasiliane nae
ReplyDeleteNaomba msaada kama kuna ndugu anajua doctor wa hili tatizo naumia sana.
ReplyDeleteNamba zangu ni 0762592558
Unamjuwa Daktari gani Bingwa wa tatizo hili pale Muhimbili?
ReplyDeleteTupe Mawasiliano yake tukamuone
Brother mungu akubariki sana umetoa maelezo mazuri ninayemgonjwa wa namna hii n.a. nimeshajua tatizo hili nitachukua hatua asante sana
ReplyDeleteKuna kusogea sawa! Vipi unapoambiwa zimesagika?
ReplyDelete