Barua ya wazi kwako baba
Pole sana baba,
Pole sana mzee wetu,
Pole sana Rais wetu Mpendwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Umefanya makubwa mno katika nyanja mbali mbali na bila kumung'unya mung'unya nathubutu kusema wewe ni mmoja wa Marais wachache mno waliofanya makubwa sana katika muda mfupi barani Afrika na naweza kusema kama itatokea taasisi ikafanya utafiti unaweza kushika nafasi ya kwanza. Ila pole sana, kwasababu moja ya mambo uliyoyatamani kufanikisha katika kipindi chako halijafanikiwa.Jambo hilo najua linakuumiza sana. Ulitamani sana kuona Soka ya Tanzania inapaa na pengine tunafanikiwa kucheza Kombe la Dunia kabla hujamaliza kipindi chako. Ila Nakupa Jambo moja lenye faraja Kuu. Nakupa ushauri ufanye jambo la kihistoria katika soka, jambo ambalo litasaidia kufanikisha taifa kufikia ndoto zako hizo muda mfupi baada ya wewe kumnaliza muda wako.
FAT ya Ndolanga ilipeleka uwezo wa Tanzania katika Soka hadi -20%, TFF ya Tenga pamoja na nguvu kubwa uliyoionesha na kuungwa mkono na makampuni makubwa na watu mbali mbali ilipeleka uwezo wa nchi katika soka hadi 0% (Ingawa wangekuwa watu muafaka kwa nguvu kubwa iliyokuwepo tungefika kwenye 35%, Hii TFF ya Malinzi kama watabadili maneno yao kuwa vitendo watapeleka uwezo wa nchi katika soka hadi 20% tu kutoka 0% tulipo. Yote haya ni kwasababu hakuna anayekuja na mikakati mizito, mikakati yote inayosemwa si mipya na si ya kipekee, haiwezi kuleta mabadiliko Chanya makubwa yanayodhaniwa na kutamaniwa.
Ushauri wangu kwako Mhe. Rais Dr. Jakaya Kikwete unda kamati maalumu ya ushauri, Ipe Muda wa Miezi 3 kufanya utafiti ije na ushauri kwako wa hatua za kuchukua kuleta mageuzi ya soka na Michezo mingine. Iwe ni kamati ndogo ya watu 5 tu iwe ni kamati ya kujitolea. Nakupa mapendekezo yangu ya watu wa kuwateua. 1.Mhe. Edward Lowassa (Mwenyekiti), 2. Mzee Reginald Mengi (Mjumbe) 3. Mhe. Nimrod Mkono (Mjumbe) 4. Mzee Idi Kipingu (Katibu) 5. Jacob Malihoja (Mimi) -(Mjumbe) Ukiacha Kipingu, kamati hii isiwe na mtu mwingine kutoka chama au taasisi yoyote inayoshughulika na michezo. Harakati zamageuzi makubwa ya soka nilizozifanya chini kwa chini kwa miaka 10 nataka kuzihitimishia katika kamati hiyo. Binafsi nahitaji kujitolea kwa ajili ya jambo hilo, lakini pia kukutana na kukaa meza moja na watu hao na pengine na wewe kwangu ni zaidi ya Mshahara au Posho. Ila mimi si lazima kuwemo kwenye kamati hiyo ila nitakuwa Tayari kutoa ushauri Bure wa nini kamati Ifanye na ifanye vipi. Maelezo zaidi ya Mpango mzima wa Kamati hiyo ifanye nini na vipi upo. Kwa Maelezo zaidi Inbox kwa inbox.
No comments:
Post a Comment