Friday, November 29, 2013

HATARI - CHINA, JAPAN na MAREKANI!

 HATARI!

China yapiga marufuku ndege Kuruka katika eneo linalogombaniwa na China, Japan, Korea ya Kusini na Taiwan ambalo lina kisiwa maarufu kinachoitwa Senkaku kwa upande wa Japan na Kwa upande wa china Kinaitwa Diaoyu. Baada ya Onyo hilo la China, Marekani na Japani zilikosoa mpango huo wa China na siku ilioyofuata Marekani ilipitisha Ndege 2 kubwa za kivita B52 katika eneo hilo, siku iliyofuata Japan na Korea ya Kusini nazo zikapitisha ndege za kivita katika eneo hilo. Kwa kuona ukaidi huo China sasa imepeleka ndege zake za kivita kadhaa kupiga Doria katika eneo hilo. Nini kitafuata?. 

Kisiwa maarufu ya Senkaku kama kinavyoitwa kwa upande wa Japan
na Diaoyu kama kinavyoitwa na Wachina,
 kisiwa hiki kipo katika eneo linalogombewa na China, Japa, Korea ya Kusini na taiwan

  Ndege za B52 zikiwa zimetandazwa katika moja ya yadi za Jeshi 
la Marekani mahali fulani nchini Marekani.

 Ndege aina ya B52 ikiwa katika matayariho ya kwenda kwenye mshambulizi

B52 ikiwa angani katika shughuli zake

B52 ni ndege Kubwa zaidi duniani za Jeshi la Marekani zinazofanya kazi karibu zote, uchunguzi, mizigo na mashambulizi. Pichani ni Ndege hizo moja ikiwa angani, moja ikiwa katika kutayarishwa na moja ikionesha moja za yadi ya ndege hizo kubwa za jehi la Marekani. Nini China inataka? Je China inatafuta njia ya kulipiza Kisasi kwa Wajapani? Je China inatafuta ugomvi na Marekani? Je China imesaua kuwa Marekani ndio iliwaokoa kutoka katika mikono hatari ya Wajapani? Nini Kinataka kutokea hapa? Sema neno mdau!

No comments:

Post a Comment