Monday, December 2, 2013

UBUYU WAWEZA KUWA HATARI


TAHADHARI.

UBUYU WAWEZA KUWA SABABU YA KUONGEZEKA KWA KESI ZA VIDONDA VYA TUMBO HASA KWA WATOTO.  UTAFITI WA HARAKA UNAHITAJIKA.


Matayarisho ya ubuyu

Kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wadogo kugundulika kuwa na vidonda vya tumbo. Jambo hili limenishawishi kufikiri kwa kina na kutafuta mahali pa kuanzia utafiti. Miaka ya nyuma ilikuwa si rahisi kusikia mtoto mdogo ana vidonda vya tumbo. Miaka ya zamani watoto walikuwa wakila vitu vidogovidogo mara kwa mara kama ilivyo kawaida ya watoto lakini miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la Matumizi ya bidhaa za ubuyu tofauti na miaka ya zamani ambapo bidhaa ya ubuyu ilikuwa haipo sokoni, ambapo ubuyu ulikuwa ukiliwa tu kwa nadra. Ubuyu umekuwa ukifungwa kwenye paketi za ukubwa tofauti na watu hasa watoto wamekuwa wakinunua sana. Ongezeko la juisi na Icecream za ubuyu nalo limekuwa ni kubwa sana na wateja wakubwa ni watoto wadogo.

Mbaya zaidi Bidhaa hii pia imekuwa ikiwekewa rangi ambazo ni kemikali. Bidhaa za ubuyu kwa sasa zinaweza kuchukua nafasi kubwa zaidi katika bidhaa ndogondogo zinazonunuliwa na watoto, jambo ambalo zamani lilikuwa halipo. Ingawa hii inatokana na hamasa kubwa kuwa bidhaa za ubuyu zina vitamini nyingi na wakati mwingine kuitwa dawa. Tofauti na bidhaa za Ubuyu, bidhaa nyingi zingine zilikuwepo tangu zamani jambo ambalo linanifanya nianze kupata wasiwasi kuwa kushamiri kwa bidhaa za ubuyu kumeanzisha ama kumeongeza kesi za watoto kuwa na vidonda vya tumbo.

Natumia fursa hii kuwataka Wizara ya Afya kuzifanyia utafiti bidhaa hizi za ubuyu na Bidhaa nyingine mbali mbali zinazowekwa rangi, na rangi na ladha za za juice  zinazouzwa hovyo kwa usalama wa Watanzania na hasa watoto. Aidha ikigundulika kweli Bidhaa za ubuyu ni dawa basi iangaliwe kiwango cha dawa na kiwango cha madhara ili ziwekewe utaratibu wa matumizi ambayo hayatakuwa na madhara. pAMOJA NA KUWA UBUYU UNATENENEZA AJIRA ZA WATANZANIA WENGI LAKINI KUNA KILA SABABU YA KUANGALIA UKUBWA WA MADHARA YAKE, MAANA TUNAWEZA KUWA TUNAINGIZA KIASI KIDOGO CHA FEDHA LAKINI UNASABABISHA KUPOTEZA KIASI KIKUBWA CHA FEDHA KUHANGAIKIA AFYA.

7 comments:

  1. Je shida Ni hiyo,rangi,au Ni ubuyu,wenyewe hebu fafanua tafadhali

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fafanua vzur mpendwa shda ni rangi au hata ubuyu wa kawaida una madhara

      Delete
    2. Fafanua vzur mpendwa shda ni rangi au hata ubuyu wa kawaida una madhara

      Delete
    3. Shida Ni rangi na syo ubuyu wenyeww

      Delete
  2. Je shida ni rangi?
    Je ubuyu Wa pilipili nap una madhara?
    Je ubuyu usio na pilipili hauna madhara?

    ReplyDelete
  3. Tufafanulie vizuri ubuyu ndo unashda Au rangi ndo inashida

    ReplyDelete
  4. Ungelezeaa rangi inanini ndani yake na ukemikali wake uko wapi hata huo utafiti ungekuwa na dira.

    ReplyDelete