Friday, January 3, 2014

MAUAJI YA TEMBO

MENO YA TEMBO YANAYOKAMATWA YATEKETEZWE HADHARANI
  • MAREKANI IMEONESHA MFANO
  • SERIKALI IIWEKEE MSIMAMO MKALI CHINA
  • CHINA WANAWEZAJE KUKAMATA MADAWA YA KULEVYA MENO WANASHINDWA?
  • OPERESHENI TOKOMEZA IENDELEE

Tembo wafanyiwa ukatili mkubwa
 
Aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii walipowkamata wachina

Na Jacob Malihoja
 Wastani wa Tembo 96 wanauawa kila siku duniani, sijui kwa hapa kwetu ni Tembo wangapi wanauawa kila siku. Wataalamu wa kimataifa wanasema tembo 35,000 waliuawa mwaka 2012 peke yake, sawa na Tembo 96 kwa siku. hii ni hali ya hatari, ni dhahiri Tanzania ni moja ya wahanga wakubwa wa tatizo hil. Mapema mwezi Nov 2013 Marekani iliteketeze meno ya tembo yenye uzito wa tani 6 ambayo yalifanikiwa kukamatwa katika kipindi cha miaka 25 iliyopita. Marekani mefanya hivyo kupinga vitendo hivyo na kutuma salamu kwa wanaofanya vitendo hivyo.
 
Kama kweli tuko Serious na tizo hili Serikali isitishe mpango wake wa kuomba ruhusaa ya kuuza meno yote yaliyokmatwa na badala yake yachomwe moto hadharani watanzania wakishuhudia huku wahusika wakishughulikiwa vikali. kwani kwa kitendo cha kupata kibali na kuyauza tutakuwa tumetumia njia nyingine ya kuwafikishia meno hayo watu ambao wamechangia kufanya ushawishi wa kuua Tembo wetu.
 
Aidha wakati huo huo Serikali ichukue hatua za haraka kuiwekea msimamo mkali Serikali ya China kutokana na tatizo la wananchi wake kuhusika kwa kiasi kikubwa na kuangamiza Tembo wetu, maana kama wao wasingekuwa wateja, kama wao wasingehitaji meno hayo hakuna mtanzania ambaye angekuwa na soko. Lakini iweje China wakawa mahili sana wa kukamta madawa ya kulevya wakashindwa kukamata meno ya tembo yanayoingizwa nchini humo? kwanini tusianze kuwa na wasiwasi na Serikali yenyewe ya China.
Na kwa upande mwingine Serikali iendelee na opereshenI tokomeza kwa nguvu kubwa lakini wahusika wakizingatia sheria na haki za kibinadamu.

NIMEANDIKA HAYA NIKIWA NA UCHUNGU MKUBWA KUTOKANA NA HALI INAYOENDELEA
IKIWA HATUTACHUKUA HATUA MADHUBUTI SASA, TEMBO NA FARU WATABAKI KATIKA VITABU VYA HISTORIA
MUNGU IBARIKI TANZANIA

No comments:

Post a Comment