CHINA YAUNGANA NA MAREKANI KUKABILI UJANGILI
YATEKETEZA TANI 6 ZA MENO YA TEMBO
China yateketeza Tani 6 za meno ya Tembo kuunga Mkono juhudi za kupambana na tatizo la Kuangamizwa kwa Tembo Duniani. Inakuwa nchi ya tatu kufanya hivyo baada ya Marekani kuanza kufanya hivyo Novemba mwaka 2013 ikifuatiwa na Uifilipino. Kwa upande wangu nimepata faraja kubwa sana kwani tarehe 3 Januari mwka huu niliweka post hapa FB nikiitaka Serikali yetu Kuteketeza meno yaliyokamatwa na Kuiwekea msimamo mkali Serikali ya China, tarehe 6 Mwezi huu (jana) China imeteketeza tani 6 za meno ya tembo na Bidhaa zake. Hata kama hatua hiyo ya China haikutokana na Maoni yangu nimefarijika sana na hatua hiyo na narudi kuisihi serikali yetu iteketeze meno ya tembo yote yaliyokamatwa kama ilivyofanya Marekani, Ufilipino na China. Kwani Meno hayo yatawafikia kwa mlango mwiongine hao hao wanaohamasisha mauaji ya Tembo nchini kwetu. Aidha serikali yetui iiwekee msimamo mkali serikali ya china juu ya wananchi wake kuhusika na ujangili huu. www.malihoja.blogspot.com
No comments:
Post a Comment