Wednesday, January 8, 2014

SEKTA YA HABARI YAPAA

SEKTA YA HABARI NCHINI YAZIDI KUPAA







Nikiwa ndani ya Studio za METRO FM 99.4 Jijini Mwanza nikiwa na Mtangazaji mahiri George Binagi GB Pazzo. Redio hii mpya inasikika kanda ya Ziwa, inafanya vizuri mno, ni tumaini jipya katika anga za habari na Burudani kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla. Kwa wakazi wa kanda ya Ziwa kama hujasikiliza radio hii basi uko nyuma ya wakati sana. Wamiliki wa redio hii na Wasikilizaji wana kila sababu ya kujivunia uwepo wa radio hii kutokana na vipindi vizuri, wafanyakazi wake kuwa watu hodari, makini na mahili katika kazi zao. Muda mfupi niliokuwa nao niliweza kuwaelewa na kuvutiwa na kazi zao. Wakanambia Wasikilizaji watarajie mambo mazuri zaidi kuanzia sasa.

No comments:

Post a Comment