Monday, March 24, 2014

RAY C MKOMBOZI WA VIJANA



RAY C NURU MPYA YA UKOMBOZI KWA VIJANA NA TAIFA.

Akiwa ameponyoka kwenye midomo ya mamba, Ray C ameamua kusimama kilimani na kupiga kelele watu wasipite eneo la mto lenye mamba!. Ray C ameanzisha Ray C Foundation kwa ajili ya kusaidia vijana na jamii kwa ujumla wajue hatari ya madawa ya kulevya sambamba na kusaidia vijana waathirika wa madawa hayo. Unapoongea nae Ray C unaweza unaweza kuona dhamira ya dhati kutoka katika sakafu ya moyo wake juu ya jambo hilo kwa manufaa ya Taifa. Akiongea kwa upole, Ray C anaonesha msisitizo mkubwa wa nia yake hiyo. Ray C anaumia sana na kuona Vijana ambao ndio nguvu kazi kubwa ya Taifa wanaathirika na mdawa ya kulevya, anasema kila anaposikia ama kumuona kijana aliyeathirika huwa anaumia sana anajua mateso aliyonayo mtu huyo.

Nilipoongea nae alinithibitishia kuwa amedhamiria na makusudio yake makuu ni kufanya uelimishaji vijana wasiingie kwenye mateso hayo ya hali ya juu na kusaidia waathirika. Anasema mapito aliyopita Mungu alikuwa na makusudio nae. Watanzania tumuunge Mkono Ray C na tumwombee afya njema, Ulinzi na malengo yake yafanikiwe kwa manufaa ya vijana wa Tanzania naTaifa kwa Ujumla. Mungu mbariki Ray C, Mungu wabariki wale wote waliomsaidia kufanikisha jambo hilo na wote watakaoendelea kumsaidia. Mungu Ibariki Tanzania. Kama Kuna Mtu ana ushauri wa jambo lolote usio na masharti yoyote atume ushauri wake kwa Ray C Foundation kwa email:  raycrayc31@gmail.com

2 comments: