Tuesday, May 27, 2014

SHUJAA RAY C

SHUJAA RAY C AANZA UELIMISHAJI

Rehema Chalamila "Ray C" akitekeleza majukumu ya asasi yake ya Ray C Foundation ameanza kupita kijiwe kwa kijiwe, Teja  kwa Teja kuwataka vijana waache madawa na wakapate matibabu Ili warudi kuwa watu wa kawaida washiriki kujenga uchumi wao binafsi, uchumi wa familia zao na uchumi wa Taifa. Ray C amewaambia vijana hao kuwa Ray C Foundation iko nyuma yao kuwaongoza, kuwashauri ili waachane na matumizi ya madawa ya kulevya ambayo ni hatari yanaharibu  mfumo wa maisha ya mtu na kuhatarisha maisha.Vijana wamfurahia na kumshukuru kwa uelimishaji, wengi waahidi kuacha.


No comments:

Post a Comment