Thursday, May 29, 2014

RAY C AUNGWA MKONO NA WABUNGE


WABUNGE WAANZA KUMUUNGA MKONO RAY C
Akionesha kufurahishwa na juhudi za Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya Rehema Chalamila "Ray C" kuelimisha vijana waache madawa ya kulevya kama alivyoacha mwenyewe na wengine wasiingie kutumia, Mhe. Cathrine Magige Mbunge wa Viti Maalumu CCM katika mchango wake Bungeni leo ameshauri Ray C aungwe mkono, ushauri huo uliungwa mkono na wabunge wengi kwa kupigiwa makofi. Ni matumaini yangu ushauri huu utapokelewa kwa vitendo na waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote wanaoguswa kwa kujitokeza na kumsaidia kwa namna wanavyoweza. Tanzania bila Madawa ya kulevya PAMOJA INAWEZEKANA. Mungu Ibariki Tanzania.

No comments:

Post a Comment