Tuesday, November 11, 2014

TUMEPAA KIUCHUMI NA MAENDELEO



TUMEPAA KIUCHUMI NA MAENDELEO
Tunahitaji Kiongozi JASIRI kuongeza kasi Zaidi na kuubadili uchumi huu kwenda kwenye Maisha ya kawaida ya wananchi wote. 

MIFANO MICHACHE NI: TANZANIA NI NCHI YA 91 KWA UCHUMI KUBWA DUNIANI (USD 33,225 MIL), YA 55 KWA MTANDAO MKUBWA WA BARABARA (91,049 KM) DUNIANI, KWA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI NI YA 24 DUNIANI (7%). KUTOKA VYUO VIKUU “SIFURI” MWAKA 1960 HADI VYUO VIKUU KAMILI 27 (11 VIKIWA  VYA SERIKALI) NA VYUO VIKUU SHIRIKISHI 22 (VITATU VYA SERIKALI) HADI KUFIKIA MWAKA 2012, KUTOKA BARABARA ZA LAMI MBILI “DAR-MORO” NA “KILIMAANJARO-ARUSHA” MWAKA 1961, HADI BARABARA ZA LAMI KUELEKEA KARIBU KILA MKOA. KUTOKA WASOMI WENYE DIGREE YA KWANZA WASIOFIKA HATA 20 MWAKA 1961 HADI KUWA NA WASOMI WENYE DEGREE YA KWANZA WANAOZIDI MILIONI 1.

Tunajivunia kilometa 91,049 za mtandao wa barabara nchini
 za lami na zilizochongwa kwa kiwango cha kokoto


 Tunajivunia ujenzi wa chuo kikubwa moja ya vyuo vikubwa barani Afrika
UDOM na Vyuo Vingine lukuki Vilivyopo nchini
 ambavyo havikuwepo hata Kimoja mwaka 1960.



Twajivunia UDSM, UDO nk.

Mafanikio haya makubwa yakisimamiwa vizuri na kwa kutumia Rasilimaali zetu Vizuri yanaweza kutupeleka kwenye 50 Bora katika Miaka 10 Ijayo.

Kwa bahati Mbaya Sana ukuaji huu wa uchumi unakumbana na changamoto kubwa ya ongezeko kubwa la ubadhilifu wa mali na fedha za Umma. Mianya imekuwa mingi na Mapanya wamekuwa wengi. Sambamba na hili Uwajibikaji na nidhamu ya kazi umekuwa wa kusuasua, uvivu katika utendaji kazi na ukiukwaji wa sheria mbali mbali umekithiri. Vitendo hivi ukichangana na wimbi la madawa ya kulevya, wizi wa maliasili, mauaji na utoroshaji wa wanyama pori, na kukosekana kwa huduma muhimu katika hospitali zetu na maeneo mengine ya huduma Taifa letu lililokuwa likimeremeta sasa linakuwa jeusi mbele ya Jamii ya kimataifa na sisi wenyewe kwa wenyewe.

Katiba inaliliwa sana lakini ukweli hata iwe katiba nzuri vipi haiwezi kujisimamia yenyewe, inahitaji utashi, Ujasiri(Uwezo wa kufanya mamuzi mgumu yenye manufaa kwa taifa na watu wake) na bunifu wa kiongozi ambaye ataapa kuisimamia na kuilinda. Anatakiwa kiongozi ambaye haindi kujaribishwa madaraka, anatakiwa kiongozi ambaye Uwezo wake katika ubunifu, utashi wa kufanya maendeleo makubwa na uwezo katika maamuzi magumu kwa mnufaa ya taifaa na watu wake umeshaonekana kwake. Kiongozi wa aina hiyo atatumia fursa ya ukuaji huu kuzidisha kasi ya maendeleo na kubadili mafanikio ya ukuaji wa Uchumi kwenda kwenye maisha ya kawaida ya Mwananchi.

Kwa Hali Iliyopo Tanzania tunahitaji mtu wa aina hiyo, Ambaye kwa Mtazamo na utafiti wangu wa muda mrefu, Edward Ngoyai Lowassa mdio Jibu sahihi. Kuna mambo machache kati ya mengi ambayo yanatoa ushahidi wa uwezo mkubwa wa mtu huyu nitayataja hapa; (1) Alipoingia Wizara ya Ardhi Mwaka 1994  (Serikali ya Ali Hassa Mwinyi) aliokoa Eneo la Serikali la Mnazi mmoja na kuwawajibisha Maafisa wa Juu wa Wizara yake ambao wao pamoja na Bilionea aliyewahonga walifikishwa kwenye vyombo vya sheria na wote kuadhibiwa kifungo na eneo kurudishwa kwenye mikono ya Serikali. ( 2) Alipokuwa waziri wa maji (Serikali ya Benjamini Mkapa) Aliasisi Mradi mkubwa wa maji (Moja ya miradi mikubwa ya maji barani Afrika) Kutoka Ziwa Victoria kuja Shinyanga na Kahama ukilenga pia kufika Tabora, Singida hadi Dodoma vikajitokeza Vikwazo vingi lakini alipigana hadi Mradi ukawepo (3) Alipokuwa Wizara hiyo ya maji alilishughulikia tatizo la Kampuni ya City Water ambao Walikuwa hawatekelezi majuku yao ilivyotarajiwa (4) Alipokuwa Waziri mkuu alisimamia kidete ujenzi wa Shule za Sekondari za kata na kusaidi Nchi kuwa na shule 3,508 mwaka 2012 kutoka shule 1,690 mwaka 2006. (5) Kutokana na mikakati yake, Ujenzi wa chuo Kikuu cha Dodoma ulianza kwa kasi ya kubwa wakati Serikali kuu ilikuwa haina fedha.

No comments:

Post a Comment