Friday, December 12, 2014


MAREKANI YAONGOZA MAJESHI YENYE NGUVU ZAIDI DUNIANI!


Ndege za kivita za Marekani zikiwa mANOARI inayoitwa 
USS Dwight D. Eisenhower katika bandari ya Marseille kusini mwa Ufaransa). 

Marekani inaongoza ikiwa na ndege za kijeshi 13,683 wanafuatiwa kwa mbali sana na Urusi ambao wana ndege 3,083 na China wenye ndege 2,788. Marekani ina manoari za kubeba ndege za kivita 10 ikifuatiwa kwa mbali na Italy yenye Manuari za aina hiyo 2, na India yenye manoari za Aina hiyo 2, China, Urusi, Ufaransa, Uingereza, Japan, Brazil, Thailand wanazo moja moja. Urusi Inaonmgoza kwa Idadi Kubwa ya vifaru vya kivita ambapo ina 15,000 ikifuatiwa na China yenye vifaru 9150 na Marekani yenye vifaru 8,325. Urusi pia inaongoza kwa Makombora ya nyuklia ambapo ina makombora 8,484 ikifuatiwa na marekani yenye makombora 7,506na kwa Mbaaali Ufaransa inafuatia ikiwa na makombora  300, china 250, Uingereza Makombora 225, nchi nyingine zenye makombora hayo ya nyuklia ni Israel inakadiriwa kuwa nayo kati ya 80-200, Pakistan Kati ya 90-110, India 80-100, Koea kaskazini Inakisiwa kuna Makombora yasiyosidi 10. Korea ya kaskazini inaongoza kwa Nyambizi (Sub-Marines) au manoari zinazopita ndani ya maji Baharini wao wanazo Nyambizi 78 ingawa inaelewa ni za teknolojia finyu na uwezo wake wa mashambulizni mwisho kilometa 4, ukilinganisha na manoari za Marekani, Urusi, China nk. Marekani inafuatia kwa idadi kubwa ya Nyambizi ikiwa nazo 72, China inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na nyambizi 69, Urusi nafasi ya nne iiwa na nyambizi 63. China inaongoza kwa idadi kubwa ya wanajeshi ikiwa na jumla ya Wanajeshi milioni 2.2. Marekani ikifuatia kwa jumla ya wanajeshi milioni 1.4 na India inashika nafasi ya 3 kwa jumla ya wanajeshi milioni 1.3http://www.businessinsider.com/the-worlds-most-powerful-militaries-2014-12
Orodha ya nchi 35 zenye majeshi makubwa duniani

No comments:

Post a Comment